01 May 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mwili wa mtoto mchanga wakutwa ndani ya boksi
 
2009-05-01 16:29:17
Na Moshi Lusonzo, Polisi Kati

Mwili wa mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya siku moja na mbili, umeokotwa katika uwanja wa mpira wa miguu Vingunguti Jijini Dar es Salaam ukiwa umehifadhiwa ndani ya boksi.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Faustine Shilogile, ameiambia Alasiri leo asubuhi kuwa tukio hilo limetokea jana, mishale ya saa 12:00 asubuhi pale kwenye uwanja huo wa mpira uliopo katika Shule ya Msingi Vingunguti.

Kamanda Shilogile amesema kabla ya kugundua mwili wa mtoto huyo, watu waliona boksi kubwa likiwa limetupwa maeneo hayo na walipoamua kulifungua, ndipo walipokuta mwili wa kichanga hicho cha kike.

Hata hivyo, akasema juhudi za polisi kumsaka mwanamama aliyefanya unyama huo bado zinaendelea ambapo akipatikana, atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Kamanda huyo amesema kuwa mwili wa kichanga hicho umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Amana.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.