05 May 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Yanga wambana Ambani
 
2009-05-05 20:43:13
By Jacqueline Massano, Jijini

Mabingwa wa soka nchini, Yanga ya jijini Dar es Salaam, imesema haitamruhusu kuondoka mshambuliaji wake Boniface Ambani kwa vile bado hajamaliza mkataba wake.

Ambani anadaiwa kufanya mipango ya kwenda kucheza soka la kulipwa na klabu ya Zheng Chang ya nchini China.

Akizungumza na Alasiri mapema leo, bosi mkuu wa Yanga, Iman Madega, alisema ameshangazwa na kauli ya Ambani ya kutaka kuondoka huku akijua bado ana mkataba Yanga.

``Ambani bado ni mchezaji wetu. Aliingia mkataba wa miaka miwili ya kuichezea klabu yetu amebakiza mmoja. Sasa anataka kwenda wapi bila kuzungumza na sisi?,`` alihoji Madega.

Madega amesema uongozi ndiyo wenye kauli ya mwisho kama mchezaji huyo aende au la na wala si kwa maneno anayoyatoa yeye (Ambani).

Bosi huyo amesema mshambuliaji huyo kutoka Kenya hakutakiwa kukaa na kuzungumza na vyombo vya habari hadi hapo watakapofanya makubaliano na viongozi wake.
``Huu ni ukosefu wa nidhamu,`` alifoka Madega.

Madega amesema kama mchezaji huyo anataka kuondokana na kwenda China aende, lakini watahakikisha hatacheza soka huko.

``Sisi ndiyo tumeshika mpini na yeye makali, kama anataka kwenda aende ila nadhani ndio utakuwa mwisho wake,`` aliongeza.

  • SOURCE: Alasiri
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.