05 May 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Daladala yapinduka, abiria 17 wajeruhiwa
 
2009-05-05 20:51:54
Na Mwanaidi Swedi,jijini

Watu 17 wamejeruhiwa vibaya baada ya daladala waliyokuwa wamepanda kupinduka. Daladala hiyo ilipinduka baada ya kugongana na pikipiki iliyokuwa inatakisha ghafla kutaka kurudi ilikotoka.

Kaimu Kamanda wa mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Aibula Tanda amesema, tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 12:50 asubuhi maeneo ya Vingunguti, Jijini Dar es Salaam.

Amesema gari hilo aina ya Toyota DCM lenye namba za usajili T 310 AWG ambalo dereva wake amekimbia baada ya ajali, lililikuwa likitokea Uwanja wa Ndege kuelekea Tazara.

Aidha amesema lilipofika eneo hilo, liligongana na pikipiki yenye namba T 487 ABW aina ya Honda iliyokuwa ikiendeshwa na Imsimili Mohamed Dada, 31.

Amesema dereva huyo wa pikipiki ambaye ni mkazi wa Kiwalani, alikuwa akitokea Tazara kuelekea Kiembe Mbuzi lakini akaamua kugeuza ghafla, ndipo alipovaana na daladala.

Baadaye, daladala hiyo ilipoteza mwelekeo na kugonga ukuta wa barabara kabla ya kupinduka.

Katika ajali hiyo abiria 17 walijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali.

Kamanda amesema dereva wa pikipiki, naye alionekana kujeruhiwa vibaya kwa kuwa alisikika akilalamika wakati wote kuwa anasikia maumivu makali mkono wa kushoto.

Amesema polisi wanaendelea kumtafuta dereva wa DCM aliyekimbia baada ya ajali kwa mahojiano zaidi.


Daladala Jijini Dar lapinduka baada ya kuvaana na pikipiki

Na Mwanaidi Swedi, Jijini

Watu 17 wamejeruhiwa vibaya baada ya kupinduka na daladala walilokuwa wamepanda ambalo awali lilivaana na pikipiki iliyogeuzwa ghafla na dereva wake ili kurejeshwa ilikotoka kwa mtindo wa `U`.

Kaimu Kamanda wa mkoa wa Kipolisi Ilala, Aibula Tanda, amesema tukio hilo limetokea jana, majira ya saa 12:50 asubuhi katika maeneo ya Vingunguti.

Kaimu Kamanda huyo amesema kuwa gari hilo aina ya Toyota DCM, lenye namba za usajili T 310 AWG na ambalo dereva wake amekimbia, lilikuwa likitokea Uwanja wa Ndege kuelekea maeneo ya TAZARA.

Akasema alipofika eneo hilo, dereva wa DCM hilo ndipo alipogongana na pikipiki yenye namba T 487 ABW aina ya Honda, iliyokuwa ikiendeshwa na dereva Mohamed Dada, 31, ambaye ni mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ofisini pale Kariakoo.

Amesema kuwa dereva huyo wa pikipiki ambaye ni mkazi wa Kiwalani, alikuwa akitokea TAZARA na ndipo alipofika Vingunguti kuelekea Kiembe Mbuzi, akitaka kurudi alikotoka.

Akasema baada ya hapo, ndipo pikipiki hiyo ilipogongana na DCM ambayo nayo ikagonga ukuta wa barabara na kupinduka.

Akasema katika ajali hiyo, abiria 17 walijeruhiwa vibaya na kukimbiziwa hospitali. Hali zao zinaendelea vizuri.

Aidha, Kaimu Kamanda akasema kuwa dereva wa pikipiki hiyo aliumia vibaya na kuwahishwa hospitalini.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.