07 May 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Simba yalegea kwa TFF
 
2009-05-07 19:06:16
By Jacqueline Massano, Jijini

Klabu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam, imesitisha maamuzi ya kuwabana wachezaji wake kujiunga na timu za mikoa kwa ajli ya mashindano ya Kombe la Taifa yanayotatarajia kuanza Mei 10.

Kabla ya maamuzi hayo yaliyotolewa jana na bosi mkuu wa Simba, mwenyekiti--Hassan Dalali, klabu hiyo ilibanwa kwa siku kadhaa na Shirikisho la Soka nchini-TFF ikitakiwa kuwaruhusu wachezaji hao kujiunga na timu walizochaguliwa.

Habari kutoka ndani ya wavaa jezi Nyekundu, zimedai kuwa, bosi Dalali jana hakuona tena sababu ya kung`ang`ania maamuzi yake ya kuwapiga `stop`wanandinga wake zaidi ya kutekeleza agizo ya watawala wa soka nchini (TFF) kuwaruhusu wachezaji hao.

Hii si mara ya kwanza kwa uongozi wa klabu hiyo kufanya maamuzi kama hayo, kwani mwaka jana hali ilikuwa hivyo huku Dalali akidai kuwa michuano hiyo haina faida kwa wachezaji wake zaidi ya kuwaingiza hasara.

Dalali alidai kuwa, michuano hiyo haithamini wachezaji na inapotokea kuumia basi jukumu la matibabu linabebwa na klabu badala ya waandaaji wa michuano.

Maamuzi ya Dalali kuwaruhusu wachezaji hao yanakwenda sambamba na mkwara kwa mikoa itakayowatumia kuhakikisha inawagharamia matibabu punde watakapopata matatizo wakati wa michuano.

Akitoa mfano, Dalali alisema michuano ya mwaka jana wachezaji Juma Nyoso na Ramadhani Kijuso hawakuweza kucheza mechi nyingi za ligi kuu baada ya kuumia na klabu ililazimika kuwatibu kabla ya kuendelea kucheza.

Bosi huyo alisema kwa sasa akili na nguvu zao wanazipeleka kwenye zoezi la usajili wa wachezaji.
Baadhi wachezaji wa Simba waliochaguliwa na mikoa kushiriki michuano hiyo ni pamoja na kinara wa mabao wa timu hiyo Haruna Moshi na mlinda nyavu Deo Mushi.

  • SOURCE: Alasiri
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.