MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  PostedComments
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Comment This Article Send this article

Aliyempiga Mwinyi afungua domo


Kwanza tunampa pole sana Mzee wetu ambaye ni Rais mstaafu Alhaji Hassan Mwinyi, kwa kitendo alichofanyiwa kweli sio kizuri hata kidogo, lakini tunapenda kumwambia asikatishwe tamaa na watu namna hiyo, tunaamini Mwenyezi Mungu atamsaidia katika yote. Mwisho Watanzania wenzangu tuwe katika hali ya utulivu na tuwasikilize wakuu wetu wa nchi wanavyosema.
  • Comment by Peter Kashaga
  • Date              Thursday 12 March 2009
  • View Original Story

Huyu kijana Ibrahim Said hajuwi misingi ya dini ya Kiislaam.Asome tafsiri ya surrat Albakrah nzima ataona kwamba dini zote ni sawa.Sisi waislaam tunawatambua mitume yote ambayo imeletwa duniani na Mnyezi mungu, kutoka Musa(Mozes), Suleimaan(Solomon),Daud, Issa bin Maryam (Jesus),Ibrahim ..... Kumpiga kofi Alhaji Mwinyi ni kosa kubwa kabisa na ni kutokuwa na adabu.
  • Comment by Dr.Khamis
  • Date              Thursday 12 March 2009
  • View Original Story

Nakupongeza sana sheikh sultan, ujumbe wako tumeupa na wale walokuwa makini na dini yao watakuwa pamoja na wewe.mungu ndio atakaye kuhukumu wewe kama kupinga zinaaa kwa mwislamu ni kosa au wale wanaoitwa ALHAJJI majina matukufu kisha yake wanasisitiza watu kufanya zinaaa kwa kutumia njia mbadala ya condom ili wafaidi vizuri tendo hilo chafu.Inasikitisha pia kwa mzee wetu kupata kadhia hiyo INSHALLAH mungu akusamehe,ila nafikiri hakukuwa na njia nyegine ya kupata ujumbe huo,kwa hiyo tunashukuru tumeupata.Hapa dunia tunapita tu ngoma ipo huko mbele baada ya mauti.

Kwa maoni yangu ,kutangaza kondom ni kuhamasisha zinaa,hilo viongozi walielewe kwamba hakuna ngono zembe wala salama.Zinaa ni zinaa.Ni dhambi.Wasisitize watu kutoikaribia zinaa. Kushirikiana katika sikukuu tunalijua toka zamani kwamba sisi watanzania ni ndugu moja,tunasherehekea na kula pamoja.
  • Comment by bilkis jiwa
  • Date              Thursday 12 March 2009
  • View Original Story

Kwa kweli kitendo ambacho amefanyiwa Rais Mstaafu Mzee Mwinyi ni kitendo cha udhalilishaji wa hali ya Juu, kwa hiyo cha kwanza ni kwamba huyo kijana inabidi achukuliwe hatua kali za kinidhamu ili liwefundisho kwa wengine. Pili kamati ya Ulinzi pia inabidi ichukuliwe hatua kali, Je kwanza tujiulize kama yule kijana angekua na siraha ya moto ingekuaje kwa kweli. CHA MSINGI NAOMBA SHERIA KALI ZICHUKULIWE KUANZIA KWA HUYO KIJANA MPAKA WALINZI WA RAIS MSTAAFU.

Nina swali kwa huyu ndugu shujaa aliyepiga: je kama yeye alichukizwa na rais mstaafu na akaamua kumnasa kibao, anaruhusu mtu mwingine aliyechizwa na kitendo cha KUPIGA achukue hatua mkononi na kulipiza kadiri atakavyoamua yeye kitendo hicho? (kama ni panga, panga; kama ni risasi, risasi nk; maana hata yeye hakuuliza mtu alipopiga)

Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.