06 May 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

JK kuhudhuria kuapishwa kwa Zuma
 
2009-05-06 20:02:41
Na Mwandishi wetu

Rais Jakaya Kikwete, kesho atakuwa miongoni mwa viongozi duniani watakaoshuhudia kuapishwa kwa Rais mpya Afrika Kusini, Jacob Zuma.

Rais Kikwete ambaye aliondoka nchini juzi usiku, leo anatarajia kuhudhuria Mkutano wa Tume ya Denmark-Afrika, unaofanyika nchini Denmark.

Akiwa nchini humo, atakutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Wamiliki wa Meli wa Denmark wakiwakilishwa na Mtendaji Mkuu na Rais wa chama hicho, Peter Bjerre-gaard.

Vile vile, Rais Kikwete atakutana na kula chakula cha mchana na Malkia wa nchi hiyo na mumewe, Prince Consort kwenye Kasri ya Fredenborg.

Anahudhuria mkutano huo akiwa ni mjumbe wa Tume hiyo ambayo Mwenyekiti wake ni Waziri Mkuu wa Denmark, Anders Fogh Rasmussen.

Wajumbe wengine wa Tume hiyo ni pamoja na wakuu wa nchi na serikali, wanasiasa, wataalam wa sekta mbalimbali, wawakilishi wa jumuia za kimataifa na kikanda na wawakilishi wa jumuia ya kibiashara, taasisi zisizokuwa za kiserikali na wasomi.

Mada kuu katika mkutano huo itakiwa ni `Vijana na Ajira katika Afrika` na ripoti ya mwisho ya Tume hiyo itaelekeza nguvu zake katika kupendekeza mkakati wa jinsi ya kuongeza nguvu za misaada ya kimataifa hasa katika maeneo ya vijana na ajira.

Vilevile ripoti hiyo itapendekeza mikakati mipya ya kupunguza umaskini, kuongeza kasi ya kukua kwa uchumi na jinsi vijana wa Afrika wanavyoweza kumiliki na kuongoza jitihada zao za maendeleo chini ya mwelekeo mzima wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa (UN).

Rais Kikwete kesho atakwenda Afrika Kusini kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Zuma baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo kupitia Chama cha African National Congress (ANC) kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Aprili 22, mwaka huu.

  • SOURCE: Nipashe
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.