08 May 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Lundenga kutembelea Miss Tabata Jumapili
 
2009-05-08 12:07:06
By Mwandishi Wetu

Kamati ya Miss Tanzania chini ya Mkurugenzi Hashim Lundenga watatembelea kambi ya Miss Tabata Jumapili katika ukumbi wa Dar West Park.

Mratibu wa Miss Tabata Godfrey Kalinga alisema jana kuwa kamati hiyo ya taifa itawafunda warembo hao kabla ya kushiriki kwenye fainali hizo ambazo zimepangwa kufanyika Mei 15 katika ukumbi wa Dar West Park.

Kalinga alisema kamati hiyo itawapa warembo mbinu mbalimbali za ushindi ikiwemo vigezo na sifa za ushindi.
Wajumbe wengine kwenye kamati hiyo ni Bosco Majaliwa (katibu), Albert Makoye (mkuu wa itifaki), Haidan Rico (ofisa uhusiano) na Yason Mashaka.

Kalinga alisema bendi ya African Stars `Twanga Pepetaí itatumbuiza siku ya fainali za Miss Tabata.
Mratibu huyo, alisema kuwa warembo 15 watashiriki baada ya mchujo huo.

Baadhi ya warembo wanaoendelea na mazoezi chini ya mkufunzi Rehema Uzuia aliyewahi kuwa Miss Ruvuma 1999 ni Zainabu Ally, 18, Latifa Amuma, 19, Rahma Bakari, 20, Everlyne Kirimbo, 22, Husna Hussein, 18, Prosperia Killian, 20, Jesca Boniface, 20, Esther Sylvester, 19, Husna Omari, 21, Jurrieth William, 18, na Sophia Almeida, 20.

Wengine ni Harrieth Mulumba, 21, Jessica Thomas, 18, Happy Romanus, 19, Fatma Bongi, 18, Mwashi Mtambo, 21, Esther Ndunguru, 20, Husna Omary, 21 and Jesca Boniface, 20.

Kalinga aliwataja wadhamini wa mashindano hayo kuwa ni Vodacom, Redds, Overmeer Wine, Freddito Entertainment, Mutesa Transport na Multichoice Tanzania.

Warembo watatu watashiriki kwenye shindano la Miss Ilala na baadaye Vodacom Miss Tanzania baadaye mwaka huu.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.