08 May 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Njia za Dar Marathon zatajwa
 
2009-05-08 12:07:45
By Faustine Feliciane

Waandaaji wa mashindano ya riadha ya nusu marathoni ya Dar es Salaam jana walitangaza njia zitakazotumika katika mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika Juni 21, mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mratibu wa mashindano hayo, John Manyama alisema mashindano hayo ya kilomita 21 yataanzia uwanja wa Uhuru hadi Ikulu na kisha kurudi Uwanja wa Taifa kwa njia tofauti.

Pia, Manyama aliwataja baadhi ya wanariadha ambao wamethibitisha kushiriki katika mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom, kuwa ni pamoja na Dickson Marwa, Victor Gatundu (Kenya), Oswald Revelin, Patrick Nyangero, Sarah Maja, Simon Patrick, Samson Ramadhan, Christopher Isegwe, Gatuli Bayo, Faustine Musa, Andrea Silvin pamoja na Martin Sule.

Manyama alisema mbali na wanariadha hao kushiriki katika mashindano hayo pia Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Joel Bendera pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Iddi Kipingu, ambao watashiriki mbio hizo kwa kilomita tano.

Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui alizitaja njia zitakazotumika zitaanzia uwanja wa Uhuru hadi Ikulu kwa kupitia barabaraba ya Mandela, Kilwa, kwenye mzunguko wa bandari kabla ya kuingia posta na kuelekea barabara ya feri hadi kufika Ikulu.

Alisema wakati wa kurudi wanariadha watatoka Ikulu kupitia barabata ya Ocean Road, watapita barabara ya Morogoro, Mnazi Mmoja, barabara ya Nyerere, TAZARA na kurudi uwanja wa Uhuru kupitia barabara ya Mandela.

Nyambui alisema ili kukwepa udanganyifu, wameweka wasimamizi katika kila kituo kwa ajili ya kunakili namba ya wanariadha watakaopita ili kukwepa udanganyifu wa baadhi ya wanariadha kutumia njia za panya ili kufika mwisho.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.