08 May 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Yanga yaanika mikakati yake
 
2009-05-08 12:08:31
By Jimmy Charles

Uongozi wa Yanga umeanika mikakati yake ya usajili, ambapo imetamba kusajili wachezaji nyota kutoka ndani na nje ya Tanzania ili kuimarisha kikosi chao.

Akizungumza na Nipashe jana, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Imani Madega, alisema kuwa kwa sasa wameamua kupumzika kufanya shughuli za klabu hiyo, ambapo mchakato wa kazi hiyo utaanza mwishoni mwa mwezi huu.

Alisema kuwa wanatarajia kufanya usajili wa `kufuru`, ambao utawashangaza wengi, ambapo hawatajali timu anayotoka mchezaji zaidi wataangalia uwezo wake na anakubalika vipi kwa kocha Dusan Kondic.

Madega, alisema kuwa hawana papara ya kujihusisha na masuala ya usajili kwa sasa, ambapo wanataka kufanya usajili wao kimya kimya, ambao utakuwa na manufaa kwa klabu yao.

Madega, aliongeza kuwa wanasubiri taarifa ya kocha wao, ambapo watakaa kuijadili na baadaye kuifanyia kazi ili kuhakikisha kuwa wanakamilisha usajili wao mapema ili kupata muda wa kujiandaa.

Alisema hana idadi kamili ya wachezaji watakaoachwa lakini inaweza kuwa ni zaidi ya wachezaji watano, ambapo maamuzi hayo yatatolewa na kocha.

Kwa upande wa nafasi za katibu, mhasibu na msemaji wa klabu wa kuajiriwa, Madega alisema masuala yote ikiwa ni pamoja na suala la kuziba nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Ngozama Matunda aliyefariki dunia, vitajadiliwa mwesho wa mwezi huu.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.