08 May 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Tumekuja kuipa `tuisheni` Stars - Wakongo
 
2009-05-08 12:09:07
By Mwandishi Wetu

Kocha Mkuu wa mabingwa wa soka wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani (CHAN), timu ya taifa ya Kongo, Muntubile Santos, amesema kuwa wamekuja nchini kuifundisha soka timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa kesho kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Nipashe jana kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo kwenye hoteli ya New Durban, Santos, alisema kuwa wanajua kuwa Stars ni timu nzuri kutokana na kuwa moja kati ya timu zilizoshiriki kwenye fainali za CHAN, lakini wao ni wazuri zaidi na ndio maana wamefanikiwa kuwa mabingwa.

Santos, alisema kuwa hawana wasiwasi na mchezo huo kutokana na kuwa na uhakika na kikosi chake, ambapo wachezaji wengi aliokuja nao walikuwemo kwenye kikosi chake kilichochukua ubingwa wa CHAN.

Alisema ingawa mchezo huo ni wa kirafiki lakini anauchukulia kama sehemu ya mchezo wa mashindano kwani anajua kuwa una umuhimu mkubwa kwa nchi ya Congo, ambapo utaweza kuwaongezea viwango vya kimataifa vya soka.

Kocha huyo aliongeza kuwa wamefurahishwa na uwanja watakaoutumia kwa ajili ya mchezo huo, ambapo wanaimani kuwa uwanja huo utawafanya wachezaji wake kucheza kwa raha.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.