08 May 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mgogoro wa ardhi wamalizika
 
2009-05-08 13:46:01
Na Salome Kitomary, Hai

Mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka saba kati ya wawekezaji wa mashamba ya kilimo cha rozela na wananchi wa Kijiji cha Mkalama, Kata ya Msama Rundugai wilayani Hai, umemalizika.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Dk Norman Sigalla,aliamua kuingilia kati na kukutana na pande zote zinazohusika na kufikia muafaka.

Chanzo cha mgogoro huo, ni wananchi wa kijiji hicho kupinga hatua ya wawekezaji wa mashamba hayo; Peter Burland na Robert, wote raia wa Ujerumani kufunga njia ambayo ilikuwa inatumiwa kuwaunganisha maeneo ya Kiwanda cha Sukari cha TPC.

Wananchi hao walisema chanzo cha ugomvi ni baada ya mfugaji wa Kimasai aliyejulikana kwa jina moja la Palmond, kuanza ufugaji kwenye shamba la Robert kabla ya mwekezaji kuanza shughuli zake na kumuondoa kwa nguvu.

Baada ya mfugaji huyo kuondolewa, inadaiwa kulitokea uharibifu wa mali za mwekezaji huyo na kusababisha hasara ya zaidi ya sh. bilioni 30, hali iliyosababisha kufungwa kwa njia hiyo.

Inadaiwa baada ya njia kufunga pande zote zilikutana bila muafaka na wananchi hawakuwa na njia nyingine ya kufika TPC ambako wanapata huduma zote.

Hata hivyo, baada ya mwekezaji kufungua njia hiyo, mali zake ziliendelea kuharibiwa na kuamua kuifunga tena kwani, hata hati kumiliki ya eneo hilo iliyotolewa mwaka 1953 haionyesha njia.

Njia hiyo ilifungwa Aprili 24, mwaka huu wananchi walijikusanya na kuzuia gari la mwekezaji kwa madai aliwazuia kupita shambani kwake na sasa hawataki apite kijijini.

Sigara alisema walichofanya wananchi hao ni makosa kwani, hati miliki ya mwekezaji haionyeshi uwepo wa njia na kwamba, iwapo wanahitaji njia ni bora viongozi wakafuata sheria.

Alisema barabara waliyozuia ni mali ya umma, hawana mamlaka nayo na mwekezaji ana haki ya kuwanyima kwani mali zake zinaharibiwa.

  • SOURCE: Nipashe
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.