08 May 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Necta yawashtukia walimu 68 Euckenford
 
2009-05-08 13:46:38
Na Godfrey Mushi

Zaidi ya watahiniwa 68 wa walimu ngazi ya cheti daraja la III A kutoka Taasisi ya Elimu ya Euckenford, wameandamana hadi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, wakilalamikia hatua ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) kuwazuia kufanya mitihani ya mwisho iliyoanza Mei 5, mwaka huu.

Kuzuiwa kwa watahiniwa hao kumesababisha vilio na simazi miongoni mwa wanachuo hao, baada ya Necta kufanya uhakiki wa mwisho chini ya kamati maalumu iliyoundwa na baraza hilo ili kupitia vyuo vya ualimu mkoani hapa.

Katika hali ya kushangaza, mmoja wa watahiniwa hao ambaye hakufahamika mara moja, cheti chake kilikutwa kikionyesha ni mwanaume, hukukumbukumbu za Necta zikionyesha ni mwanamke tangu alipofanya mtihani wa kidato cha nne.

Wanachuo hao waliokuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kujifariji, huku wengine wakiangua vilio walisema walimu wataficha wapi nyuso zao, walifikisha malalamiko yao kwa Afisa Elimu Mkoa wa Tanga, Julius Mhanusi.

Akizungumzia hatua ya Necta, Mhanusi alisema watahiniwa 68 ndio waliofikisha malalamiko yao kwa maandishi ofisini kwake na nane walihakikiwa na kuruhusiwa kufanya mtihani.

Alisema walilazimika kufanya uhakiki upya chini ya kamati maalumu toka Necta, huku watahiniwa 44 kati ya 68 waliowasilisha malalamiko yao wakikosa sifa.

``Kamati iliwaita na kuwatangazia kila mmoja wao alete leaving certificate, lakini kati ya hao 68, wanachuo 24 ndio waliojitokeza mbele ya kamati na kufanyiwa uhakiki upya…baada ya ukakiki wa kina nane walikuwa na sifa na kuruhusiwa kufanya mtihani,``alisema Mhanusi.

Hata hivyo, baadhi ya wanafunzi waliozungumza kwa sharti la kutotajwa, walisema wanashangazwa na hatua ya baraza kukaa kimya muda mrefu hadi kipindi cha mtihani wa mwisho.

Mkuu wa Chuo cha Ualimu Euckenforde, Dominick Katto, alisema hana jibu la malalamiko hayo bali wenye mamlaka ya kuzungumzia jambo hilo ni Necta.

  • SOURCE: Nipashe
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.