30 Apr 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Vijiji zaidi ya 34 vimepatiwa vyandarua vyenye dawa Nkasi
 
2009-04-30 20:47:57
Na Radio One Habari

Wananchi wa vijiji thelathini na vinne wilayani Nkasi mkoani Rukwa, wameanza kupatiwa vyandarua vilivyotiwa viuatilifu vinavyotolewa na mradi wa afya ya msingi Ziwa Tanganyika, ili kukabiliana na ugonjwa wa malaria.

Chini ya mradi huo kila kaya katika vijiji hivyo itapewa bure vyandarua viwili ambapo kwa kuanzia kijiji cha Korongwe kimepatiwa vyandarua elfu sita mia nne.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya Dakta Alex Ndenge amesema kumekuwa na uelewa mdogo juu ya matumizi ya hati punguzo, kwani wananchi wanakataa kupokea vocha hizo kwa madai kuwa hawana fedha za kuongezea.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Bwana Daniel Ole Njoolay ameyapongeza makundi yaliyofanikisha mradi huo na kuwataka wananchi kuvitumia vyandarua hivyo.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.