26 Apr 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

AFC wataka kuchaguana
 
2009-04-26 14:00:32
By Mwandishi Wetu

Uongozi wa zamani wa timu ya AFC ya Arusha kesho Jumatatu utamuona mkurugenzi wa manispaa ya mji huo na Afisa Utamaduni, ili wapange taratibu za kuitisha uchaguzi wa klabu hiyo kongwe.

Katibu msaidizi wa zamani, Peter Zayumba alisema kwa njia ya simu kuwa uongozi wa zamani umeamua kuuona uongozi wa juu wa serikali ili kuinusuru timu hiyo.

Zayumba alisema hivi karibuni uongozi huo wa serikali ulitoa maamuzi ya kukutana kwa uongozi wa zamani na kamati ya muda iliyokuwa imeteuliwa na mkuu wa wilaya aliyehamishwa hivi karibuni Evans Balama, ili kuweka wazi mapato na matumizi waliyotumia katika kuhudumia timu hiyo iliyoshiriki fainali za ligi daraja la kwanza na kushindwa kupanda daraja.

``Hawa wanakamati tumewaambia tukutane nao kwa siku ya tatu hawajaonekana na ndio maana tunarudi kwa mkurugenzi na afisa utamaduni, ili atoe maamuzi mengine kwani sisi tunataka kuendeleza timu yetu na sio malumbano,`` alisema Zayumba.

Alisema kamati hiyo inatakiwa kuweka wazi mapato na matumizi ya sh. milioni nane zilizokuwa zimetolewa na watu mbalimbali kwa ajili ya kuihudumia timu hiyo, ambayo hata hivyo inadaiwa iliishi kwa shida ilipokuwa katika kituo cha fainali jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia maandalizi ya timu hiyo pekee iliyokuwa tishio kwenye miaka ya 2002 katika ligi kuu kwa kuvifunga vigogo vya soka nchini, Simba na Yanga, alisema wataanza usajili mapema Julai kwa ajili ya kushiriki ligi hiyo itakayofanyika Agosti.

AFC iliyokuwa ikiundwa na wachezaji chipukizi ilijikuta ikishindwa kupanda daraja baada ya kushika nafasi ya nne na kuziacha African Lyon, Majimaji ya Songea na Manyema Rangers zikienda Ligi Kuu.

  • SOURCE: Lete Raha
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.