26 Apr 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Ligi ilikuwa ngumu - Kaseja
 
2009-04-26 14:02:06
By Bahati Mollel

Kipa nguli nchini, Juma Kaseja wa Yanga amesema ligi ya msimu huu ilikuwa ngumu na yenye ushindani mkubwa tofauti na ligi nyingine zilizopita.

Kaseja aliliambia LeteRAHA ugumu huo uliongezwa chachu kwa wachezaji kuwa na ushindani binafsi, na pia timu kwa timu nazo zilikuwa zikishindana ili kujiweka katika nafasi nzuri kimsimamo.

``Ligi ilikuwa ya kiwango cha juu, timu zilipishana kwa pointi chache na kila mmoja alijitahidi kumpita mwenzake ili awe juu katika msimamo,``alisema Kaseja.

Alisema ushindani huo uliwalazimisha timu yake ya Yanga kucheza kwa bidii ili kujikusanyia pointi mapema kabla ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza.

``Sisi tulicheza tukiwa na taswira ya ule usemi wa biashara asubuhi na ndio maana tulichangamka na kumaliza mzunguko wa kwanza tukiwa na pointi nyingi zaidi ya timu nyingine, na hata mzunguko wa pili uliendelea hivyo hivyo,`` alisema Kaseja.

Akitoa mfano wa ushindani na kiwango cha juu cha soka katika mojawapo ya mechi ni kilichoonyeshwa mwishoni mwa wiki na watani wa jadi Simba na Yanga, ambapo wachezaji walionyesha mchezo mzuri usiokuwa na rafu za makusudi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

``Mimi nimecheza mechi za watani nyingi, lakini sikuwahi kuona mechi nzuri kama hii iliyopita wachezaji wamecheza kwa nidhamu na hata soka lilionekana, na ndio maana wapenzi walifurahi kwa kuona soka zuri lisilokuwa na vurugu,`` alisisitiza Kaseja.

  • SOURCE: Lete Raha
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.