03 May 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Nurdin, Naftal waomba kuchezea Arusha KT
 
2009-05-03 18:47:54
By Mwandishi Wetu

Walinzi Nurdin Bakari wa Yanga na David Naftal wa Simba ni miongoni mwa wachezaji 10 wa ligi kuu ya Bara walioomba kuchezea kikosi cha mkoa wa Arusha kwenye michuano ya Komba la Taifa iliyopangwa kuanza Jumapili ijayo kwa hatua ya makundi.

Kocha mkuu wa timu ya mkoa wa Arusha Madaraka Bendera aliliambia Lete RAHA kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki kuwa Bakari na Naftali wameomba kuchezea timu yake.

Bendera ambaye aliwahi kuwa kocha wa Simba mwaka 2007 alisema mbali na wachezaji hao wawili, Meshack Abel wa Simba, Kigi Makassy, Amir Maftaha wa Yanga na Chesido Methew wa Villa Squad pia wameomba kuchezea Arusha.

Idadi ya wachezaji 10 wa ligi kuu ya Bara walioomba kuchezea Arusha inakamilishwa na Abdallah Juma wa Kagera Sugar, Habib Mhina, Salvatory Ntebe na Erasto Nyoni wa Azam, alisema Bendera.

Wachezaji hao watachujwa leo Jumapili ili kubaki na watano kwa mujibu wa kanuni za Kombe la Taifa, alisema ambazo haziruhusu zaidi ya wachezaji watano wa ligi kuu ya Bara kwenye timu ya mkoa mmoja.

Bingwa wa michuano hiyo mwaka jana timu ya Ilala iliyokuwa ikifundishwa na Jamhuri Kiwhelu ilitumia kikosi cha kwanza cha Simba.

Aidha Pwani ilitumia kikosi cha JKT Ruvu jambo ambalo lilizusha mang\'uniko kwa mikoa iliyokuwa haina timu za ligi kuu.

Bendera alisema baada ya mchujo timu itaendelea na mazoezi ya wiki moja.

Arusha ni mwenyeji wa Kundi D pamoja na timu za mikoa ya Mara, Kilimanjaro na Manyara na haitarajiwi kushindwa kuingia robo-fainali zitakazofanyika Dar es Salaam.

Mbali na Arusha vituo vingine vya michuano hiyo itakayomalizika Mei 30 ni Mbeya, Tanga, Mwanza, Ruvuma na Dodoma.

  • SOURCE: Lete Raha
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.