03 May 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Ambani kutoacha pengo Yanga 2010
 
2009-05-03 18:48:55
By Bahati Mollel

Kocha mkuu wa mabingwa wa soka wa Bara Yanga Dusan Kondic amesema hakutakuwa na pengo lolote katika timu hiyo msimu ujao endapo mshambuliaji wake hatari Boniface Ambani atakwenda kucheza soka la kulipwa nchini China.

Ambani ambaye ameibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya Bara akiwa na mabao 18 aliliambia Lete RAHA katika mazungumzo maalumu jijini mwishoni mwa wiki kuwa Kondic amemhakikishia hakutakuwa na pengo Yanga.

Alisema Kondic amesema lengo la klabu hiyo ni kununua na kuuza kwa faida wachezaji mahiri ndani na nje ya nchi.

``Baada ya kushinda majaribio nilijaribu kuongea na kocha juu ya nafasi yangu katika timu, lakini alinihakikishia hakutakuwa na shida kwani wana uhakika wa kupata wachezaji wengine bora zaidi wa kujaza mapengo ya watakaokuwa wameondoka,`` alisema Ambani.

Ambani alikwenda kwenye majaribio ya kucheza soka nchini China mwanzoni mwa mwezi uliopita na akafuzu.

Kabla ya kusajiliwa Yanga, Mkenya huyo alikuwa India.
Kama atakwenda China Ambani atajiunga na timu ya Hangzhou Greentown.

Aliyekuwa mlinda mlango namba moja misimu miwili iliyopita Ivo Mapunda aliuzwa kwa mabingwa wa Ethiopia St. George kwa dola za Marekani 9,000 (sawa na zaidi ya shilingi milioni tisa) msimu uliopita.

Mlinda mlango wa Yanga Obren Curkovic kutoka Serbia pia anadaiwa kutaka kusajiliwa na SuperSport ya Afrika Kusini msimu ujao na winga machachari Mrisho Ngassa anataraji kufanya majaribio ya pili na West Ham United ya Uingereza katikati ya mwaka.

Mlinzi Nadir Haroub `Canavaro`, inadaiwa, anasubiri kwenda katika majaribio ya kuichezea Vancourer Whitecaps ya Canada itakayoshiriki ligi kuu ya Marekani, MLS, mwakani.

Ambani alisema anamsubiri wakala wake Alex Bandom wa Afrika Kusini awasili kukamilisha mazungumzo ya mwisho na uongozi wa Yanga.

  • SOURCE: Lete Raha
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.