03 May 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Ratiba Kombe la Taifa kupangwa leo
 
2009-05-03 18:51:10
By Mwandishi Wetu

Ratiba ya mashindano ya Kombe la Taifa la mikoa yaliyopangwa kuanza Mei 10-30 kwenye vituo sita itapangwa leo na kamati ya mashindano ya shirikisho la soka, TFF, itakapokutana jijini Dar es Salaam Katibu mkuu Frederick Mwakalebela alisema jijini jana Jumamosi kuwa .

Mashindano hayo yataendeshwa kwa ligi katika hatua ya awali ya makundi na timu nane zitafuzu kucheza robo-fainali.

Mashindano hayo yatashirikisha timu 23 zikiwa zimeganywa katika makundi sita katika vituo vya mikoa ya Mbeya, Tanga, Mwanza, Arusha, Ruvuma na Dodoma.

Mikoa mingine itakayoshiriki ni Rukwa, Iringa, Ilala, Pwani, Kinondoni, Kagera, Kigoma, Shinyanga, Mara, Kilimanjaro, Manyara, Temeke, Lindi, Mtwara, Tabora, Singida na Morogoro. Ilala ndio bingwa mtetezi wa michuano hiyo.

Mwakalebela alisema mbali na ratiba ya mashindano hayo, pia kamati hiyo itajadili michezo ya kufunga pazia ya ligi kuu ya Bara iliyomalizika Aprili 27.

``Watapitia ripoti za waamuzi na makamisaa kwa kuangalia kama kutakuwa na adhabu kwa wachezaji na waamuzi pia, ili waweze kuzitoa kwa mujibu wa kanuni,`` alisema Mwakalebela.

  • SOURCE: Lete Raha
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.