03 May 2009 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Kaseja no tena Simba-Dewji
 
2009-05-03 18:54:39
By Waandishi Wetu

Kamati ya usajili ya klabu ya Simba itakuwa na mamlaka ya kutoa ushauri tu kwa mwalimu kazi hiyo itakapoanza mwezi ujao, lakini haitakubali kurejeshwa kikosini mlinda mlango namba moja nchini Juma Kaseja, imeelezwa.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Kassim Dewji alisema jijini juzi Ijumaa wamekubaliana kwamba kocha Patrick Phiri ndiye atakayewasilisha mapendekezo ya usajili na kamati hiyo itamshauri.

Pamoja na kwamba kamati yake haina nia ya kumuingilia Phiri, lakini haitarajii kupitisha usajili wachezaji walioikimbia msimu uliopita kwa madai ya kutafuta maslahi zaidi.

``Hatutaki kumuingilia kocha kabisa, ila tutatoa mapendekezo yetu.`` alisema Dewji na kueleza zaidi, ``sio lazima (kocha) ayakubali mapendekezo yetu.``

``Tunafanya hivyo kuhofu huenda (kocha) akawa hajamuona mchezaji fulani... kamati itampendekeza lakini kama kawaida kabla ya usajili kutakuwa na muda wa majaribio.

``(Lakini) sidhani kama wale waliokimbilia maslahi kwingine wanaweza kuwa na nafasi tena Simba,`` alisema Dewji.

Kaseja aliondoka Simba msimu uliopita na kujisajili na Yanga kwa dau la shilingi milioni 30 ambalo limemfanya mlinda mlango huyo kuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya ligi kuu ya Bara.

Mbali na Kaseja, beki kiraka Nurdin Bakari pia alisajiliwa na Yanga na kwa pamoja kuisadia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu ikiwa na mechi tano mkononi.

``Sisi hatuna uwezo mkubwa wa kifedha kwa hiyo sio rahisi kuwapa fedha nyingi kama zinavyotolewa na wenzetu wa upande wa pili,`` alisema Dewji.

``Kipaumbele tunawapa hawa waliopo sasa kwani ndio wenye mapenzi na moyo na timu yetu, si unakumbuka wapo waliokuwa wakisemwa wangejiunga na Yanga lakini tunao hadi leo?``

Kiungo Henry Joseph na beki Kelvin Yondan walikuwa wakitakiwa kwa udi na uvumba na Yanga pia mwaka jana lakini Simba ikafanikiwa kuwabakiza.

  • SOURCE: Lete Raha
Comment on this article
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.